GET /api/v0.1/hansard/entries/1135730/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135730,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135730/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Prof.) Ongeri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 124,
"legal_name": "Samson Kegeo Ongeri",
"slug": "samson-ongeri"
},
"content": "Nawashukuru wenzangu kwa kupitisha hoja inayowania kuongeza bujeti kwa serikali zetu za ugatuzi. Nitarajia kwamba wakati Wizara ya Fedha itakapo tangaza bajeti mwaka ujao, watatia maanani pendekezo zilizowasilishwa na maseneta leo bila kutafuta mbinu za kushusha kiwango cha fedha kilichopitishwa na Bunge hili leo. Nina imani kuwa serikali za kaunti hazitapata chini ya Kshs485 bilioni. Waziri wa Fedha atakapo leta makisio ya bajeti, tunatarajia kuona kwamba yote tuliyopendekeza yamewekwa katika bajeti bila tashwishi lolote. Pili, siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 zimeanza na nimeona kwamba wanasiasa wengi wana tabia ambayo haiwezi kuleta amani katika nchi hii. Nawasihi wanasiasa wenzangu watulie kidogo katika harakati za kisiasa ile tuwe na mikakati za kuleta uwiano na amani. Tusitenganishe watu kwa mambo ambayo hayawezi kutujenga. Matamshi yetu katika kampeni yawe ya kulenga umoja na kujenga bali si kubomoa nchi. Pia, ningependa huwasihi wabunge na viongozi wote wa nchi wawe na heshima. Kama unaenda kutembea katika eneo la mbunge mwingine, unapaswa kumpa kiongozi wa eneo hilo heshima na sio kueneza siasa za uchochezi. Nawasihi wanasiasa wote tuwe wataratibu katika mienendo yetu na njia zetu za kisiasa wakati huu wa sherehe za Krismasi na mwaka mpya. Bw. Spika, nakushukuru kwa kutupa mwelekeo mzuri mwaka huu. Tumekuwa na vikao kadha wa kadha mwaka huu na hivyo tukaweza kuhitimu mambo mengi. Itakuwa fanaka kubwa mwaka ujao tutakaporejea vikao vya Seneti. Nina imani kuwa tutapitisha miswada na hoja zilizobaki kwa maana zina maana sana kwa watu wetu. Haja yetu ni kuboresha maisha ya wananchi wa Kenya katika kaunti zetu ili wananchi wetu haswa vijana, kina mama, wazee na wachuuzi waweze kukuza na kuboresha biashara zao zaidi ya hali ilivyoko sasa. Mwisho, ningependa kuwakumbusha wananchi wote kwamba bado tunapambambana na janga la COVID-19. Virusi vya COVID-19 vya Omicron ni hatari. Virusi hivyo vinaenea haraka sana kama moto uliowashwa katika kichaka kilichokauka. Nawasihi wananchi wote wajiatharishe zaidi wanapoungana na wenzao. Ugonjwa huo wa COVID-19 umeleta maafa mengi katika jamii zetu. Nawasihi maseneta wenzangu na wakenya kwa jumla kujikinga na COVID-19 kwa sababu ugonjwa huo utaturudisha nyuma zaidi. Bw. Spika, nachukua fursa hii kuwatakia watu wote wa Kaunti ya Kisii na wakenya wote kwa jumla krismasi njema na mwaka mpya wenye heri."
}