GET /api/v0.1/hansard/entries/1135733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1135733,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135733/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa nakupongeza wewe na ofisi yako kwa kazi njema ambayo mumefanya mwaka huu. Umetuongoza vyema katika vikao vya Seneti ambavyo tumekuwa navyo mwaka huu. Pili, nawashukuru maseneta wenzangu kwa ushirikiano mwema ambao wamenipa tangu nilipojiunga na Seneti. Mimi si mchanga kwa umri lakini mimi ni mchanga katika Bunge la Seneti. Nilipokelewa vyema hapa Seneti nilipojiunga mwezi wa tatu. Tangu nilipojiunga, nimeweza kuwasilisha arifa mbali kuhusu mambo yanayowaathiri watu wa Kaunti ya Machakos. Nina imani kuwa arifa hizo zitapitishwa hivi karibuni na kwamba Kaunti ya Machakos itaweza kuorodheshwa kama mojawapo ya eneo zenye ukavu. Kaunti yangu ya Machakos inaendelea kukumbwa na shida ya ukosefu wa maji. Natarajia kwamba swala hilo litakapowasilishwa hapa Seneti, litapitishwa na vile Bunge la Taifa. Bw. Spika, nawashukuru maseneta wenzangu kwa kupitisha miswada nyingi sana hii tuliyopitisha leo inayolenga kuongezea serikali zetu za kaunti fedha ili waeze kufanya kazi vizuri. Nina furaha kwamba tumepitisha fedha kiasi cha Kshs485 bilioni iendee kaunti zetu ili kufaidi watu wetu. Nawasihi magavana kwamba watakapo pokea pesa hizo, wafanye kazi vilivyo ili wasaidie wananchi wa kaunti zao. Hizo pesa zikifika, tunaomba magavana waweze kufanya kazi inayofaa kwa ajili ya wananchi."
}