GET /api/v0.1/hansard/entries/1135738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135738,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135738/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, nikimalizia, wakati huu wa Krisimasi madereva wengi huenda kwa mwendo wa kasi. Kwa hivyo, ninawaomba waendeshe wananchi kwa usalama ili tusipoteze maisha. Ninawatakia watu wangu wa Kaunti ya Machakos na Kenya kwa jumla, Krisimasi njema yenye baraka za Mwenyezi mungu na mwaka mpya wenye mafanikio. Ninaomba Wizara ya Elimu na wahusika wote wafanye kila juhudi ili wazazi wanaporudisha watoto shuleni mwezi wa kwanza, watoto wanaotoka kwa familia ambazo hazijiwezi wapate bursaries ili wazazi washughulike na vitabu na uniforms. Huu wakati ni mgumu sana kwa sababu ya Covid-19; biashara nyingi haziendi vizuri kama ilivyotakuwa kabla ya Covid-19. Kwa hivyo, tujali masilai ya watu wetu na tusaidiane inavyostahili. Bw. Spika, ninakutakia wewe, Maseneta na wananchi wote Krisimasi njema. Ninaomba tufanye siasa za amani. Wanaosimama kuchaguliwa kama Rais waelekeze watu vyema. Wananchi pia wachague viongozi ambao watasaidia. Ninatumai tutarudi wote hapa mwezi wa pili tukiwa salama na tutamaliza mwaka vizuri."
}