GET /api/v0.1/hansard/entries/1135742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135742,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135742/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii ya kuwa wa mwisho kuzungumza. Ninawatakia Wakenya wote salamu za heri na fanaka msimu huu wa Krisimasi. Ninaomba demokrasia iweze kudumu ili kila mtu awe na haki ya kujieleza kwa uhuru. Katika msimu huu wa Krisimasi, tuwe na umoja na tuweze kusaidia wale ambao wana kipato cha chini na hawajafaidika kama wengine. Pia tudumishe undugu ndiposa kila mtu ajihisi kama Mkenya. Tusiangalie tofauti zetu za kisiasa kama jambo la kututenganisha sisi kwa sababu tutakuwa na mirengo mingi ya kisiasa, upande huu utavutia upande ule mwingine. Lakini fauka ya hayo yote, Kenya nzima inafaa kujiendeleza na kujizatiti kwa manufaa ya kila mwananchi. Pia, ninawahimiza viongozi kutoa misimamo ambayo ata kama itatofautiana kisiasa lakini isilete pingamizi au tofuati za kuwagawanyisha Wakenya. Bw. Spika, ninakushukuru kwa uongozi wako katika muhula huu wote wa Bunge la Seneti ambao tumeumaliza. Huu ni muhula wa tano katika awamu hii ya Bunge. Hii inamaanisha tumebakisha miezi michache tumalize Bunge la pili la Seneti. Ninatumai kwamba Wakenya watapiga msasa kuangazia utendakazi wetu na kutupa nafasi za kuendelea kufanya kazi katika Bunge hili, lile lingine au katika kitengo kingine cha uongozi katika nyanja za kijamii. Ninakushukuru na tuwe na Krisimasi njema na mwaka mpya wenye mafanikio."
}