GET /api/v0.1/hansard/entries/1135743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1135743,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1135743/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Lusaka",
"speaker_title": "The Speaker",
"speaker": null,
"content": " Nami ninachukuwa nafasi kushukuru Bunge la Seneti kwa jumla kwa ustadi na kwa kusimama kama Bunge moja licha ya mawimbi mbalimbali ambayo yalitokea msimu huu. Tumekuwa na mambo mengi lakini tumekaa pamoja kama Bunge la Seneti. Ninawashukuru sana kwa Miswada ambayo mmeleta ambayo inakinga ugatuzi na kwa maswala ambayo tumezungumzia. Ninajivunia kama Spika wenu kwa kuongoza viongozi ambao wamekomaa na kuchangia sana kukua kwa ugatuzi katika Jamuhuri yetu ya Kenya. Sitasahau kushukuru viongozi ambao tunafanya nao, haswa Viongozi wa Waliowengi na Waliowachache na wote walio katika Senate Business Committee (SBC). Ninawashukuru kwa sababu pamoja tumefanya kazi kwa kushirikiana na kuorodhesha maswala ambayo yamekuwa yakizingatia sana mambo ya ugatuzi katika nchi yetu. Ninashukuru pia secretariat wakiongozwa na clerk na wote ambao wamehakikisha tumekuwa na vikao bila shida yeyote. Ninamatumaini kwamba Mungu akitupa uhai, tutakutana tena Februari na kuendelea kufanya kazi yetu. Kama vile Maseneta wengine wamesema, tuendelee kuzingatia kanuni za afya kwa mambo ya Covid-19. Haswa tukienda mashinani, lazima tuhakikishe kwamba sisi kama viongozi, tuko kwenye mstari wa mbele kuelimisha watu wetu juu ya ugonjwa wa Covid-19."
}