GET /api/v0.1/hansard/entries/1139269/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1139269,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1139269/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nataka kumpomgeza Seneta Shiyonga kwa Mswada huu wa marekebisho ya sheria ya KEMSA. Kwa kweli umekuja wakati unaofaa kwa sababu ukitembelea KEMSA, utapata kuwa hata dawa ambazo wako nazo ni asilimia 60 pekee yake. Kwa hivyo, kaunti zetu zikijaribu kuagiza dawa unapata dawa nyingi hazipo. Kisheria, ni vigumu kwa kaunti zetu kununua dawa kutoka mahali pengine. Ukitembelea hospitali zetu kwa mfano Hospitali kuu ya Nanyuki au Nyahururu, unapata kuwa hakuna dawa. Unapata watu wanaishi maisha ya uchochole kwa sababu ya ukosefu wa dawa. Tungependa dawa zipatikane kwa bei nafuu katika hospitali za Serikali. Mambo yanayohusu afya yako katika gatuzi zetu, ni jukumu letu kama Seneti, kama vile Sen. Shiyonga ameleta Mswada huu, mimi ninaunga mkono. Ukiangalia bei ya dawa katika hospitali zetu inakuwa wanaponunua pale KEMSA ni bei maradufu kwa sababu hakuna ule ushindani. Ikiwa kuna ushindani kama vile inapendekezwa katika Mswada huu, basi Wakenya wataweza kupata mahali watanunua"
}