GET /api/v0.1/hansard/entries/1139271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1139271,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1139271/?format=api",
    "text_counter": 173,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "dawa katika hospitali zetu kwa bei nafuu kwa sababu kaunti zilinunua dawa hizi kwa bei nafuu. Kwa hivyo, naunga mkono. Jambo lingine ambalo ningependa kusema ni kwamba ikiwa afya imeletwa katika gatuzi zetu, inapaswa hata KEMSA yenyewe iweze kuletwa katika gatuzi zetu. Hii ni kwa sababu utapata mtu anasafiri kutoka Rumuruti kuja kununua dawa Nairobi. Hii inachukua muda mrefu sana. Haya marekebisho yamekuja wakati unaofaa kusaidia kaunti zetu. Kaunti zetu zitanufaika ikiwa Mswada huu utapitishwa na mimi nitauunga mkono ili tuweze kuupitisha. Ukitembelea KEMSA, unapata dawa zilizoko huko zimekaa sana kwa sababu kuna taratibu nyingi ambazo zinazingatiwa ili dawa ziweze kufika katika kaunti zetu. Unapata ya kwamba inachukua muda mrefu sana. Unapata kuwa dawa ambazo ziko hapo ziko karibu kuharibika. Kwa hivyo, wakati zinafika katika kaunti unapata zimebakisha miezi miwili au mitatu ziharibike. Wananchi wanasema hawana imani na zile dawa kwa sababu zimebakisha miezi miwili ili ziharibike na wanazitumia kwa taharuki. Mswada huu utaleta maridhio mema katika kaunti zetu. Nataka kuunga mkono na kusema kuwa umekuja wakati mwema. Namshukuru na kumpongeza tena Seneta Shiyonga. Asante."
}