GET /api/v0.1/hansard/entries/113930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 113930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/113930/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bi Naibu Spika wa Muda, naomba nichukue nafasi hii nitoe pongezi zangu kwa Rais kwa Hotuba aliyotoa wakati wa kufungua Bunge majuma mawili yaliyopita, na kwa kielelezo alichokitoa kuhusu mwelekeo anaotarajia Bunge kufuata wakati wa kuchangia mjadala wa Katiba mpya. Ni muhimu Wakenya wakae na watafakari na wajiulize wao wenyewe: âJe, Katiba tunayotarajia kuitengeneza ni ya watu gani? Ni ya Wakenya wanaoishi hivi sasa ama ni ya vizazi vijavyo? Haina haja ya watu kuudhiana ama kutiana udhia. Ni muhimu watu watafakari na kuelewana. Wakristo wakae chini waelewane na Waislamu. Haina haja hata kidogo ya watu kuzozana. Nia yetu ni kuhakikisha kwamba tumepata Katiba ambayo itaweza kuiendeleza nchi yetu kama inavyotakikana. Nikikumbuka vile Rais alivyosema, ni matarajio yake kuona kwamba nchi inaendelea mbele na inapata viwango vya ustawi kama inavyohitajika. Lakini tukumbuke kwamba viwango vya ustawi vitakua ni shida kupatikana kama yale matukio yaliyotufanya tukazozana mwaka wa 2008 hayataangaliwa kwa undani na kwa ujasiri na kufikiriwa vile yakavyoweza kutatuliwa. Bi Naibu Spika wa Muda, uchumi wa nchi hii hauwezi kwenda mbele iwapo mambo kadha wa kadha hayatachunguzwa. Nikitaja machache, tuanze na mambo ya barabara. Imebainika wazi kwamba kila Mbunge aliyesimama hapa kuchangia Hotuba ya Rais kwa Bunge, amelalamika na kulia kuhusu barabara mbovu katika eneo la Bunge analowakilisha. Tukumbuke kwamba kilio hiki kinaletwa na mambo ambayo yametokea hapo awali. Ukiangalia hivi sasa Mkoa wa Pwani, kwa mfano, utaona kwamba barabara ya kutoka Voi kwenda Taveta imeisha. Kila Rais ambaye amechukua usukani wa nchi hii ameahidi kwamba atarekebisha barabara hiyo. Rais Moi alisema vivyo hivyo, lakini hamna lolote lililotokea. Rais Kibaki akaja, akasema vivyo hivyo, lakini hamna lolote lililotokea. Hivi ninavyosimama hapa, hiyo barabara imeisha kabisa. Magari hayawezi kupita. Mnatarajia wale watu wafanye nini? Tunavunjana moyo na hisia kama hizo zikiachwa zikiendelee kupanda, itakuwa vigumu sana kwa watu wa Kenya kukubali kuwa wako pamoja na wanaendelea pamoja. Usambazaji wa raslimali umekua ni pengo kubwa katika nchi hii. Tuanze na mahospitali. Katika tarakimu zilizotolewa na Serikali yenyewe, inabainika wazi wazi kuwa katika miaka minne iliyopita, Mkoa wa Pwani ndio ulipata fedha chache zaidi kuliko mikoa mingini kukidhi maswala ya afya. Je, ni kwa nini? Tukiwauliza wakuu wa Serikali wanasema: âHayo ni makosa ambayo yamepita.â Kwa nini yakubaliwe yapite? Je, tuna hakikisho gani kwamba kuanzia sasa, madhambi yanayotendewa watu wa Pwani yatakomeshwa? Haya ndiyo mambo ambayo tunatakiwa tutafakari na kujiuliza: âJe, tuko wapi na tunaelekea wapi?â Kuna swala kama lile la Mzima Springs. Maji yanatoka Mzima Springs, katika eneo la Taita nzima, kabla kugawanywa na kuwa wilaya za Taveta, Wundanyi, Voi na Mwatate. Maji hayo yanaenda mpaka Mombasa. Watu wa Mombasa hawayanywi hayo maji bure. Wanayanunua. Hizo fedha zikilipwa, zinaenda wapi? Hazirudi pale kuboresha hudumu hiyo ama angalau, kuanzisha bomba la pili la maji. Zimekua zikitokomea tu; miaka nenda, miaka rudi. Hivi sasa, watu wa Mombasa wanalia kwamba hawana maji na maji yako chungu nzima Mzima Springs. Kwa nini tusiwe na mabomba mawili ya mifereji ya maji? Huu ni ufisadi ama ni nini? Kero yao ni nini?"
}