GET /api/v0.1/hansard/entries/113931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 113931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/113931/?format=api",
    "text_counter": 277,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Tukiangalia mambo ya mbuga za wanyama, tunapata ziko Taita lakini hakuna faida yoyote watu wa huko wanapata. Tukianzia Taveta hadi Tsavo Magharibi, hakuna kitu watu wa huko wanapata. Tukija Taita mlimani ambapo pia kuna Tsavo Magharibi na Tsavo Mashariki, tunaona hawapati chochote. Je, mambo kama haya yataendelea mpaka lini? Tukiulizana nini kinachoendelea, hakuna mtu anayetueleza kinachoendelea. Ninaomba tuulizane mambo yaliyotokea baada ya kura ya mwaka wa 2007. Mambo ya ardhi yalitajwa kuwa moja ya mambo ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa watu kuzozana na kupigana. Tunayashughulikia namna gani mambo haya? Rais alisema kwamba angependa watu wawe na maridhiano. Sawa. Je, ni mwelekeo gani tunauchukua kuhusu jambo hili? Tume ya Mariadhiano imeweka mambo gani ya kushugulikia maridhiano? Je, watu wa Kenya wameridhiana sasa hivi ama bado kuna utata? Ni maoni yangu kuwa mpaka sasa hakuna shughuli kabambe ambazo zimeandaliwa ambazo zitawafanya watu wa Kenya waridhiane na wasameheane. Hata tupitishe sheria gani, kama watu hawataridhiana na kusameheana na kuondoa chuki, tutakuwa tunawasha ule moto uliokuwa hapo awali. Bi. Naibu Spika wa Muda, ni ombi langu kwamba wakati umefika watu wa Kenya kukaa chini, tuulizane: Jamani, matatizo kama haya sisi wenyewe hatuwezi kuyatatuwa? Nina imani tunaweza kuyatatua. Katika kazi na ufisadi, unakuta kuna kazi zilizobuniwa nchini kupitia mpango wa Kazi kwa Vijana.Tukiangalia vile vijana walivyoajiriwa pia, tunapata kuna dosari. Vijana walikuta wengine wameajiriwa na hakukuwa na mtu wa kueleza vijana hao wameajiriwa kivipi. Ukiuliza vijana hao wametoka wapi, unaambiwa ni mpango wa Serikali. Lakini ni utaratibu gani ambao ulifanywa kuhakisha kwamba Mpango wa Kazi kwa Vijana umetekelezwa na kila sehemu, watu wamepata haki yao? Mara nyingi hapo ndiyo tunakosea. Tunabuni miradi, mawazo ni mazuri, miradi yenyewe ni mizuri lakini tukija kwa utekelezaji unakuta dosari. Hizi dosari ndizo zinafanya kila wakati Serikali ionekane machoni mwa wananchi kuwa haifanyi kazi inavyotakikana. Tunakubaliana kuwa nchi hii inakumbwa na ufisadi. Kutokana na habari tunapata kila wakati, tunaona kwamba watu na Wizara fulani zimehusika na ufisadi. Lakini imekuwa ni vigumu kuwaona hao watu wakichukuliwa hatua zinazoonekana. Ni hivi sasa tumeona ufisadi katika City Council of Nairobi kuhusiana na ununuzi wa pahali pa makaburi. Ni hivi sasa hatua imechukuliwa. Shilingi milioni 257 zilizotumiwa badala ya shilingi milioni 24 zimechukuliwa na watu wachache. Haya ndiyo mambo yanayowaudhi watu wa Kenya. Ni hatua gani inatakikana kuchukuliwa? Bi. Naibu Spika wa Muda, mfumo wa elimu wa hivi sasa unaadhirika kwa sababu pesa ambazo zingetolewa na mataifa wafadhili zimebanwa kwa sababu kuna ufisadi katika nchi hii. Je, ni sheria gani tutabuni katika Bunge hili kuhakikisha ufisadi umekomeshwa? Tunakubaliana kuwa vyuo vikuu vinafanya viwesavyo ili viboreshe elimu nchini. Lakini mara nyingi unakuta kuna kasoro fulani. Hakuna usawa katika wale ambao wanachukuliwa katika vyuo vikuu. Unakuta wengine wamechukuliwa kutoka sehemu fulani na wengine hawakuchukuliwi. Katika kuajiriwa kazi, utakuta wengine walichukuliwa sehemu fulani na wengine hawakuchukuliwa. Ni kitu gani kinaendelea nchini? Ni ombi langu kwamba Bunge likae na lije na njia mwafaka ili janga la ufisadi liangamizwe kabisa nchini mwetu, ili lisiwe janga ambalo litakuwa linatuletea utata. Bi. Naibu Spika wa Muda, ni msimamo wangu kuwa rasilimali lazima zisambazwe kote nchini. Hii ndiyo maana mfumo huu wa kusambaza fedha kupitia maeneo ya Bunge unahakikisha kwamba watu wamepata haki yao."
}