GET /api/v0.1/hansard/entries/1142562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1142562,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1142562/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ni jambo la kusikitisha kwa ripoti ya Mwenyekiti kuja hapa na kuwa kama ripoti ya kawaida. Hususan ni kwamba Mkenya ama wakenya wamepoteza Maisha yao. Tunatarajia ya kwamba taarifa kama hiyo ambayo imeletwa hapa mbele ya Bunge iwe imeshikilia, inaweza kutegemewa na kutufikisha mahali pa kutuambia aliyetenda kitendo hicho, kwa sababu gani, na hatua gani itachukuliwa na serikali. Jambo la kusikitisha leo ni kwamba huyu mama anayeitwa Joannah aliuwawa na imekubalika kuwa aliuwawa. Lakini baada ya hapo ni hatua gani imechukuliwa kuona ya kwamba wale watu waliofanya kitendo hicho cha kinyama wamechukuliwa hatua. Maneno kama haya vilevile yametokea katika sehemu mbalimbali za nchi, ama maeneo ya Pwani hususan Mombasa. Ni jambo la kusikitisha kuona mpaka sasa vijana zaidi ya ishirini wameweza kupotea Mombasa na hawapatikani. Jambo ambalo limedhihirika wazi ni kwamba miili ya watu saba imepatikana. Miili sita kati ya saba zilizopatikana haijawezakutambuliwa na jamaa zao. Mwili moja iliyotambuliwa, ilipatika katika mto wa Yala. Visa hivi vya Wakenya kupotea hasa vijana, alafu miili yao kupatikana katika mto wa Yala zimekidhiri zaidi. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba mto huo unatumiwa; kutupa watu waliofariki, waliouwawa mahali pengine na kutupwa huko, ama tayari wamechukuliwa na magari wamezamishwa wamefungwa na hawawezi kuongea wala kufanya chochote wakiwa ndani ya magunia. Kisha wakatupwa ndani ya mto hiyo ambapo hawawezi kuogelea wakiwa ndani ya magunia. Ni hali ya kutetesha sana kwa sababu maisha ya Wakenya ni muhimu. Haiwezekani mtu kushikwa leo na kesho tunaambiwa amepatikana Yala kutoka Mombasa, Kilifi ama sehemu zozote za Kenya, si haki. Tunatarajia ya kwamba Mwenyekiti wa Kamati hii ya Usalama wa Taifa, Ulinzi na Mahusiano ya Mataifa za Kigeni awe akija kwenye Bunge la Seneti na kutuletea ripoti mwafaka ambayo inaweza kutueleza ni njia gani mwafaka inaeza tumiwa kusitisha mambo kama hayo. Polisi wanaweza chunguza ni watu wagani ambao wanaotenda vitendo vya kinyama na kutupa watu ndani ya mito kama mto wa Yala wamepatikana na hatua imechukuliwa."
}