GET /api/v0.1/hansard/entries/1142632/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1142632,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1142632/?format=api",
"text_counter": 128,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Kwanza, ningetaka kuunga mkono huu Mswada wa marekebisho katika unyunyizaji wa maji. Ukulima ni uti wa mgongo wa nchi yetu ya Kenya. Hususan Mswada huu ukiwa unahusika na unyunyizaji wa maji, ni jukumu muhimu sana katika nchi yetu ili kuona kuwa tumeweza kukuza chakula cha kutosha ama mimea ambayo inaweza kuzaa vyakula vya kutosha ili kustahimili Wakenya. Haya ni kwa sababu tunakumbwa na janga la njaa mara kwa mara. Kwa hivyo, hii ni sekta ambayo itawasaidia Wakenya kwa muda mrefu."
}