GET /api/v0.1/hansard/entries/1142653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1142653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1142653/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, sijui ni kwa nini tunajibizana na Kiongozi wa Walio Wengi na mimi ninaongea kuhusu upande ambao ninafahamu vizuri na ni eneo langu. Shamba hili sasa limepata mabwenyenye. Serikali imekata mapande nakugawanya ilhali watu wanaoishi pale, hawajapewa mashamba. Iko kesi kubwa sana ambayo tumeleta kwa Serikali ya kwamba wenyeji wapewe shamba katika maeneo ya Galana Kulalu ambayo ina pande mbili. Galana iko Kilifi na Kulalu iko Tana River. Kwa hiyo, lazima awezekuelewa yale maeneo. Maneno hayo sasa yanajibishiwa kwa hali ya kwamba watu wanazungumza lakini iweze kugawanywa kisawasawa na wakaaji wa pale wapewe hanki. Kama ni Wagiriama, wapewe mashamba yao. Hii ndio sababu nakwambia, hiyo biashara ya kwamba Galana Kulalu inazaa mazao imesimamishwa kufikia hivi sasa. Hivi sasa, ndio watu wako katika zile njia za kuweza ku-i dentify wale wakaaji wamaeneo wapewe maeneo yao na kule kutabaki, Serikali inaweza kuleta watu wengine. Bado hatujakubali hayo maneno. Ukae ukijua hivyo."
}