GET /api/v0.1/hansard/entries/1143552/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1143552,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1143552/?format=api",
    "text_counter": 386,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie jambo hili muhimu na maana la historia ya Bunge. Kusema ukweli, hapo mwanzoni labda hakukuwa na Wabunge Kenya. Lakini kuna ile siku kulikuwa na utekelezaji wa maendeleo hasa maendeleo ya kisiasa tukitumia Bunge kama kielelezo ama barabara ya kuwa na uwiano na maendeleo ya kisheria na kiuchumi. Kama hakuna historia ambayo watu wanawezaangalia, basi tutakuwa tumepotea. Nashukuru wale wamekuwa na fikira kama hizi na kuona ni muhimu kukuza historia ya Bunge. Katika maendeleo ya Bunge hili, tuzingatie viti na vipasa sauti tunavyotumia hivi sasa. Wakati tulipoanza, tarakilishi haikuwa pale. Lakini kwa sababu ya utaratibu na teknolojia ambayo imekuwa ikionekana na kutekelezwa katika nchi zingine, sisi pia tukajiandaa ili kujaribu kufikia wale ambao wako mbele yetu. Kama hakukuwa na historia ya pahali watu wametoka au pahali maendeleo yamekuwa, basi ingekuwa vigumu sana kutekeleza mabadiliko. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii. Naomba wale walio na ujuzi, hata wale wako nje ya Bunge hili, waungane nasi ili tuweze kutengeneza historia nono ambayo itaelekeza Bunge letu mbele. Shukrani kwa kunipatia nafasi ya kunena hayo."
}