GET /api/v0.1/hansard/entries/1144024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1144024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144024/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": " Bw. Spika, ndugu yangu anasema kuwa ni wale ambao walikuwa pale mbeleni ndio wameendelea kuwa katika hii Kamati. Lakini nataka ajue ya kuwa Sen. Madzayo aliteuliwa juzi kuwa mwanachama wa Kamati hii wakati ambao tulianza kipindi hiki . Hakuwa mwanachama hapo zamani. Sen. Kwamboka pia alikuja juzi kama yule Seneta ambaye aliteuliwa na African National Congress (ANC). Sen. Moi amekuwa mwanachama wa Kamati hii muda wa miezi sita iliyopita. Pia Sen. Sakaja na Sen. Kibiru waliteuliwa hivi majuzi. Sen. Olekina amekuwa katika Kamati hii kwa muda wa mwaka mmoja lakini amefanya kazi nzuri sana. Sijui kama Seneta anadhani kuwa hawajafanya kazi kikamilifu. Kama kuna mambo mengine, basi ayaseme. Juzijuzi tulikuweka kitini, hata hakuna kurudisha asante. Kweli asante ya punda ni mateke."
}