GET /api/v0.1/hansard/entries/1144028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1144028,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144028/?format=api",
    "text_counter": 72,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, Sen. Orengo ananikanganya kwa sababu nimemsikia akitaja kiti cha ufalme. Sikujua tuna kiti cha ufalme katika Bunge hili. Ni mara yangu ya kwanza kusikia juu ya kiti hicho, lakini ni vizuri vile ambavyo ameniarifu. Vile nilikuwa nikimaanisha ni vizuri kujumuisha Maseneta wale wengine ili waweze kuwa na uzoefu wa kuendesha shughuli za Bunge. Mimi sipingi Hoja hii. Sisemi ya kuwa Sen. Olekina si mjuzi, si mtu aliyebombea katika kazi yake; si mtu ambaye haelewi kazi yake; ni mtu ambaye anaifahamu kazi yake vilivyo. Nilisema ni vizuri wengine wahusishwe, sisemi wale walioko hawafanyi kazi yao vizuri. Ninaunga mkono. Asante, Bw. Spika."
}