GET /api/v0.1/hansard/entries/1144724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1144724,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144724/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumpongeza Mhe. Barasa kwa kuja na Mswada huu. Pia, tumeona kuwa watu wengi wanafanya kazi na baadaye, wanaishi katika ufukara. Vilevile, wengine wanakufa kabla ya kupata marupurupu yao. Mhe. Barasa amefanya vizuri katika Mswada huu kwa kuwa yatakikana mtu akifika kustaafu, kabla hata hiyo miezi mitatu haijafika ndio aanze ile mipangilio ya kufuatilia hii pesa, ni muhimu Serikali ishughulikie mambo haya ili mtu anapostaafu, anapewa pesa na malimbikizi yake yale anayostahili kupewa mara moja. Pia, tuanona kuwa kumefanyika ugatuzi kwa mambo mengi. Kwa hivyo, kwenye marupurupu, ingekuwa bora zaidi pia badala ya wao kuja kuhangaika hapa Nairobi maana pengine, hawajui ofisi yenyewe na wanapata shida ilhali hawana mahali pa kukaa, ni muhimu yule anayestaafu ikiwa yuko mkoa fulani, aweze kupata peza zake pale. Ninampongeza Mhe. Barasa."
}