GET /api/v0.1/hansard/entries/1144761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1144761,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144761/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Leo, tarehe 2.2.2022, nikiwa katika mkutano wa kamati, nilipatiwa habari ya kusikitisha na kuhuzunisha sana, ya kuwa katika eneo la Old Town, kuna moto mkubwa ulioweza kutokea na watu sita wamepoteza maisha yao. Kwa hivyo, tunavyozungumza, kuna mama na mtoto wake wanapata matibabu katika hospitali iliyoko karibu. Hamna badili ya maisha, na hata tukaweza kuzungumza vipi, hakuna njia ya kuregesha maisha ya walio aga. Hakuna lile ambalo tunaweza kulisema likawa ni dawa ya lile donda la moyo ambalo liko kwa wale waliopoteza watu wao. Sio watu wao pekee yao, bali ni watu wetu sote. Ni kuomba tu Mwenyezi Mungu panapo majaliwa yake awaweke pema palipo na wema. Mwenyezi Mungu awajalie waliopoteza watu wao na awape badala njema, Inshallah."
}