GET /api/v0.1/hansard/entries/1144776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1144776,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144776/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kukitokea jambo lolote, mkasa ama jambo kama lile lilitokea pale Mvita, wahudumu hawa ndio watu wa kwanza tunawaona wanakimbia kuokoa maisha ya wananchi. Vile vile kama tunavyoelezwa na jina lenyewe, wako kabisa mashinani kwa jamii. Wanatembea hata wakati tumekumbwa na ugonjwa wa Corona. Wanashikana na machifu, wazee wa mitaa na wengine wengi sana kuangalia matatizo yanayopatikana kwa watu. Wanakimbia katika vijiji lakini hawalipwi, hawapewi motisha, na hawapewi nguvu yoyote. Wanafanya kazi katika hali ngumu sana kwa sababu hawana vifaa, na vile vile wakati wa kuwapatia taluuma ya kuangalia vile wataweza kuondoa shida zilizoko katika sehemu zetu, inakuwa ni shida. Wanafanya kazi katika mazingira hatari sana. Leo ukienda Coast General Hospital, wengi wanaowasaidia watu ni wahudumu wa afya wanaopeleka wagonjwa huko."
}