GET /api/v0.1/hansard/entries/1144777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1144777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144777/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kama wenzetu walivoyosema, ni wakati mwafaka hivi sasa kuona kwamba bajeti ya Kenya inatenga pesa za kuwasaidia wahudumu wa afya wa jamii. Nataka kubatiliza katika Mswada huu ili kuzungumuzia wengine kidogo. Sio wahudumu wa afya wa jamii pekee yake. Hata mabalozi, wazee wa mitaa wanafanya kazi kubwa, lakini tukiangalia chifu na mkuu wa tarafa, wanaonekana wamefanya kazi kumbe imefanywa na wazee wa mtaa na balozi ambaye yuko pale. Kwa hivyo, ni muhimu kuona kuwa watu kama hawa wanaofanya kazi nyanjani wanapewa motisha na pesa. Pesa nyingi zinapotea nchini. Zinapotea kwa sababu ya ubadhirifu wa pesa unaoonekana. Ubadhirifu wa pesa ulionekana hata juzi katika kiongozi wetu wa chama cha ODM. Alisema akichukua urais, atafinya sehemu zote ambapo pesa zinapotelea ili kuhakikisha kwamba pesa zinafika nyanjani kuwasaidia watu kama hawa."
}