GET /api/v0.1/hansard/entries/1144790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1144790,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144790/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": "Watu wanaohudumu katika nchi hii kwa njia ngumu na ya matatizo ni wahudumu wa afya wa jamii. Mswada huu ukipata nafasi ya kufika kwenye Bunge hili ni kwa sababu sisi ni wawakilishi, na kule chini nyanjani sisi ndio tunaona vile hawa wafanyikazi ambao wamejitolea wanavyofanya kazi. Mazingira yao ni magumu na hawana vifaa vya kufanya kazi. Kama juzi wakati wa Corona, hawa ni kati ya wale wafanyikazi waliojitokeza kuwa tayari kuhudumia wananchi kwa njia yoyote. Kwanza, walikuwa wametia maisha yao kwenye hatari. Pili, walikuwa wamejitolea kwa sababu kila tunapo ondoka katika mitaa yetu ama katika sehemu tunazoishi kwa sababu pengine mmoja ama wawili wameweza kujisaidia, kwa kweli walijitolea."
}