GET /api/v0.1/hansard/entries/1144791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1144791,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1144791/?format=api",
"text_counter": 310,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lungalunga, JP",
"speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Sisi, kama Bunge la Kitaifa, tuko na nguvu ya kupanga bajeti na ya kutatua maswala yanayotoka nyanjani. Lakini, kwa maswala kama haya ambayo wale wanaotokwa na jasho jingi katika nchi hii ni wale walio nyanjani, kwa mfano, c ommunity health workers, w azee wa mitaa na mabalozi wa vijiji…Mfano mzuri ni kama kobe. Unajua kobe akicheza, ndani yuko kama mkakasi. Akiwa anapiga ngoma, atapiga ngoma kule ndani lakini huwezi kujua kama anacheza mpaka uone jasho linamtoka. Hao wafanyikazi, c ommunity health workers, wanafanya kazi kubwa sana kwa sababu sehemu tunazotoka ni sehemu ambazo, kwa mfano, hazina barabara na d ispensaries zilizoko ziko mbali mbali. Urahisi wa kuweza kufanya mambo haya na kuhakikisha afya ya mwananchi ni sawa ni kuwapa nguvu ili waweze kuhudumu zaidi. Katika kila tunacho fanya au chochote afanyacho mwanadamu huwa anategemea apate fidia au malipo. Kwa nini sisi, kama Bunge la Kitaifa, hatuwezi kukamilisha swala hili na tuhakikishe kuwa c ommunity health workers,w azee wa mitaa pamoja na mabalozi wamepate fidia kwa kazi wanayofanya? Katika usalama, wao ndio huleta maswala yoyote kuhusu usalama. Ikiwa kuna jambo linalotakikana katika vijiji, wao ndio hutoka na kuyazungumza. Kwa hivyo, nasimama kwa dhati kuunga Mswada huu mkono, na kusisitiza kuwa isiwe kama yale mazungumzo tunayopiga kila siku. Sisi, kama Bunge la Kitaifa, tunatakiwa tuwe na nguvu ya kuhakikisha tunayasukuma maswala haya yafanyike ili wizara husika isikise Mswada utakaopitishwa na Bunge hili. Ni muhimu kwa c ommunity health workers wapatiwe vifaa wanavyohitaji . Ingawa maswala ya afya yamegatuliwa kikamilifu, swala kama hili la kuhakikisha kuwa wale walio nyanjani kama c ommunity health workers, wameangaliwa na Serikali kuu, yafaa iwe kitengo kivyake. Tukisema tuachie counties kwa sababu limegatuliwa, tutapata matatizo makubwa. Sasa hivi, pesa za counties zinakuja kidogo kidogo na kunakuwa na gap . Katika hiyo gap, utapata wafanyikazi wanakaa miezi mitatu au minne bila malipo. Kwa hivyo, tuliondoe swala hili kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for informationpurposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}