GET /api/v0.1/hansard/entries/1145344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1145344,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1145344/?format=api",
    "text_counter": 66,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika. Nimefanya kazi kwa Ministry of Health (MOH) kule Elgeyo Marakwet. Ofisi yangu ilikuwa katika sehemu inayoitwa Chebiemit. Sehemu hii ya Kerio Valley imekuwa na shida kwa muda kutokana na mambo ya wizi wa ng’ombe na wananchi kupoteza maisha yao. Nimesikia majibu ambayo Mheshimiwa Mwathi ameleta kutoka kwa Waziri. Aliongea kuhusu maafisa wa NPR na kusema kuwa kuna mpangilio wa kuwafanyia vetting . Ikiwa watu wa Kerio Valley wanaumizwa na matukio yanayotendeka, kusema kuwa kuna mpangilio ya kufanya vetting ni kudhulumu wananchi hao na kuwaacha kama hawana Serikali. Kwa hivyo, namuomba Mheshimiwa Mwathi aangalie mambo ambayo Waziri amesema kwa sababu sio haki. Maafisa wa NPR wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika Jamhuri yetu ya Kenya. Walisimamishwa kazi kule Kerio Valley tangu mwaka wa 2018. Sehemu nyingine kama kwangu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}