GET /api/v0.1/hansard/entries/1145345/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1145345,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1145345/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
"speaker": {
"id": 1458,
"legal_name": "Robert Pukose",
"slug": "robert-pukose"
},
"content": "Endebess, maafisa wa NPR wanafanya kazi lakini hawapokei yale marupurupu madogo waliokuwa wanapewa. Ni vizuri kuangalia maswala ya maafisa wa NPR katika sehemu ambazo wananchi wana hatari ya kushambuliwa na wezi wa ng’ombe. Ni muhimu pia maafisa wa NPR wapewe silaha na kulipwa marupurupu madogo ya kuwasaidia kufanya kazi nzuri. Naomba Serikali yetu ichukulie kwa uzito mambo ya usalama katika sehemu ya Kerio Valley na sehemu nyingine kama vile Baringo na mipaka ya nchi yetu. Tunapoelekea katika msimu wa uchaguzi, ni vyema kuhakikisha kwamba kila Mkenya anaishi salama salmini na mali yake. Si vizuri kuwacha hawa wezi wa ng’ombe washambulie wananchi. Kwa hivyo, namuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Usalama arudi kwa Waziri na kumwambia kuwa kama Wabunge, hatujaridhika na yale majibu ameleta na achukulie jambo hili kwa umuhimu lililo nalo kwa sababu ya usalama wa Wakenya. Asante, Mheshimiwa Spika."
}