GET /api/v0.1/hansard/entries/1145360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1145360,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1145360/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": " Asante Mhe. Spika. Nilipokua ninachangia huu Mjadala, Daktari mmoja aitwaye Benjamin Kibor alinitumia ujumbe kwamba tunapoongea sasa hivi, kuna mashambulizi yanayofanyika katika Eneo Bunge la Mhe. Bowen, mahali panaitwa Kabetwa. Tayari, mtu mmoja ashauawa. Mashambulizi yanaendelea hata sasa hivi, tunapoongea. Kuna kituo cha Polisi kinachoitwa Mogil, pale Kabetwa. Pia, tuko na kituo cha GSU kule Tot. Mhe. Pkosing anavyongelea, ni mbali na mpaka. Iko katikati ya Marakwet Magharibi kuelekea upande wa Baringo. Kwa hivyo, tunapoongelelea mambo ya usalama; kuna wezi upande wa Pokot na Marakwet. Tusiangalie tu maisha ya binadamu vile Mhe. Pkosing anavyosema mambo ya usawa. Mambo ya usawa haihusikani na mambo ya usalama. Kila mmoja anahitaji kulindwa; maisha ya kila Mkenya ni ya muhimu sana. Kwa hivyo, tusifikirie kuongelelea mambo ya usawa wa usalama ila, tuangalie kila Mkenya, awe upande wa Pokot ama Marakwet, wajue wanalindwa vilivyo."
}