GET /api/v0.1/hansard/entries/1146421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1146421,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1146421/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuungana na wewe katika kuwakaribisha marafiki wetu kutoka Uchina na wanafunzi wa Acacia Crest Academy. Ningependa wanafunzi na walimu kutoka shule ya Acacia Crest Academy wajue ya kwamba sio kawaida yetu kuwa wachache hivi katika vikao vyetu vya hapa Seneti. Kisa na maana ni kwamba tumo katika msimu wa siasa. Kwa hivyo, Maseneta wengi hawako hapa. Hili ni jambo ambalo wanafunzi na walimu wanapaswa kulifahamu. Najua mmekuja kusoma mengi yanayotendeka katika Seneti. Ikiwezekana, mrudi tena wakati ambapo msimu wa siasa utakuwa umekwisha ili musome na mfahamu kwa mapana na marefu jinsi shughuli za Seneti zinavyotekelezwa na Maseneta wenu. Ninawapa changamoto wanafunzi hawa kwa sababu leo sisi ndio tuko hapa lakini nyinyi ndio mtakuwa hapa kesho kama viongozi. Ninawasihi muweka bidii katika masomo yenu kwa sababu masomo ni uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu. Pia ninawasihi muige yale mazuri mutakayoyaona viongozi wakiyafanya. Sisi tunawaangalia nyinyi kwa sababu katika maendeleo yoyote ya nchi, wanafunzi ndio tegemeo kubwa. Masomo mueke mbele na pia mfuatilie jinsi mambo yanafanywa humu nchini. Baadaye nyinyi ndio mtaendesha sekta mbalimbali humu nchini na kuleta maendeleo zaidi. Ninawaomba mtilie maanani yote mliokuja kusoma hapa. Hatimaye, ninaomba radhi tena na pia ni hofu kidogo kwa sababu mmekuja wakati ambapo hatuko wengi hapa kwa sababu ya msimu wa siasa. Hata hivyo, mkija wakati mwingine kama Seneti imejaa, mtaweza kusikiza jinsi mijadala inavyojadiliwa katika Bunge la Seneti."
}