GET /api/v0.1/hansard/entries/1147336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1147336,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147336/?format=api",
    "text_counter": 639,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naungana na wenzangu kupongeza Kamati husika kwa kuja na Ripoti hii. Kwa kweli, utakubaliana na mimi kwamba suala la afya ni nyeti na muhimu sana. Nawashukuru kwa kuwa wamelizingatia kikamilifu na kuliwekea mikakati. Mengi yamezungumzwa na wenzangu kuhusiana na suala hili. Masikitiko makubwa ni kwamba ni kweli sisi Waheshimiwa tuko na zile kadi za bima ya afya. Lakini, utapata kwamba unapopatikana na matatizo ukiwa hapa Bunge ama sehemu nyingineyo, huna budi kukimbilia hospitali kujiangalia afya. Kuna mambo mengine ambayo unapaswa kupitia hata kabla hujafika hospitali. Tukiwa hapa Bunge, Waheshimiwa huwa na kazi nyingi katika shughuli zao. Vilevile, wanapitia mambo mengi hapa na pale katika suala nzima la kuendeleza shughuli zao za kawaida. Kwa hivyo, itakuwa vyema kuweko na kitengo maalum. Hata ikiwezekana, kuwe na sehemu maalum ya hawa madaktari ama wahudumu hapa Bunge ambapo Waheshimiwa wanaweza kufika wakati wowote na kuangalia mambo madogo madogo ya afya yao. Mfano ni kupima presha, kupima sukari na mambo madogo madogo ambayo naamini humbidi mtu atoke aende hospitali akapige foleni. Kukipatikana kitengo hiki ambacho kitakuwa kimewekwa katika Majengo haya ya Bunge kwa sababu hii, itasaidia pakubwa na litanufaisha. Vilevile, kwa maoni yangu, sitaki jambo hili liwe ni pendekezo la Waheshimiwa tu. Kwa sababu afya ni jambo muhimu, ingekuwa bora jambo hili lifikishwe hata mashinani. Kwa masikitiko makubwa, utapata ni wengi wanakuwa na shida sana kujielewa wana matatizo gani. Ni kwa sababu hawawezi kufikia huduma hizi za kujiangalia afya. Pengine mtu anajua hospitali iko lakini kufika kule na kuanza kujiangalia inakuwa changamoto. Utapata kwamba pengine Serikali ina ule utaratibu wa kuwafikishia watoto chanjo mahali walipo. Malengo haya ni kuhakikisha watoto wamepewa chanjo kwa sababu ya magonjwa yanayochipuka. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}