GET /api/v0.1/hansard/entries/1147337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147337,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147337/?format=api",
"text_counter": 640,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Katika sehemu nyingi za nchi hii na kaunti zetu, utapata watu ni wagonjwa lakini hawawezi kufikia zile huduma za kujua magonjwa yao. Ndiposa utapata mtu amekaa na mara presha imepanda ila hajui alikuwa nayo; mtu amekaa, amepatikana na matatizo haya na hajui. Kwa hivyo, itakuwa vyema ikiwa Kamati itaangalia haya mambo zaidi na kuhakikisha kuwa kaunti zetu ziko na huduma za madaktari wa kutembea kama wale wanaopeana chanjo kwa watoto wadogo. Ukifanya utafiti wako, nchi hii yetu iko na watu wengi wanaoathirika na madhara ya afya ilhali hawajui. Itakuwa bora tukipata serikali yenye mipangilio ya kuenda mashinani kuangalia afya za wananchi pale wako. Sio lazima mtu aende hospitalini kujua hali ya afya yake. Tunafaa kuwa na utaratibu wa kufuata watu mahali walipo. Suala la afya ni muhimu sana na tunahitaji kulizingatia. Ningependekeza kuwe na kituo maalum na wahudumu wa kisawasawa hapa Bunge. Mtu akiwa na matatizo yoyote au akihisi kuangalia afya yake, sio lazima atoke kwa Bunge na kuenda hospitali ya Aga Khan au Pandya. Anafaa kujua kuna sehemu ya kuenda na kujipima kujua hali yake. Dharura yoyote ikitokezea, badala ya kukimbizwa moja kwa moja mpaka hospitali, kuwe na sehemu hapa ya mtu kupata huduma ya kwanza. Baada ya hapo ndio utaratibu ufanyike wa mtu kupelekwa hospitali. Litakapopatikana hili nina imani tutakuwa tumeweka miundo msingi ya kuhakikisha kwamba afya yetu imeangaziwa kikamilifu. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii. Na inafaa kupanuliwa zaidi ndio badala iwe ni masuala ya Wabunge peke yao, iwe inashughulikia masuala ya wananchi wote. Utaratibu unafaa kutafutwa wa kuangalia afya ya wananchi kwa namna moja au nyingine. Asante."
}