GET /api/v0.1/hansard/entries/1147403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147403/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Khaniri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 171,
"legal_name": "George Munyasa Khaniri",
"slug": "george-khaniri"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, hata hivyo ninakubali kukosolewa na Sen. Faki. Nilikuwa nasema ya kwamba wamepata nafasi za kuja kujifunza mengi kwa Bunge la Seneti. Nashukuru ya kwamba uongozi wa Kaunti hiyo inawapatia nafasi hiyo. Seneti ni mahali pazuri pakuja kujifunza. Tuko na mila na tumaduni njema za kuigwa. Kwa hivyo, mnajifunza kutoka kwa wale ambao wamebobea katika taaluma yao. Kwenu siwezi jitetea. Nilijitetea kwa wageni wa kutoka mbali kuwaeleza ya kwamba Seneti hii viti vinaoneka bila watu kwa sababu watu wamekimbia mashinani kutafuta kura. Nyinyi ni wa hapa n mnaelewa ya kwamba hii sio kawaida yetu. Wengi wanatafuta njia za kurudi hapa; wengine kama mimi wanataka kuwa Magavana. Ninawania kiti cha Ugavana wa Vihiga. Kwa hivyo, hii sio kawaida yetu. Tunawakaribisha na tunawatakia kila la kheri kwa wiki ile moja mtakayokuwa hapa. Asanteni."
}