GET /api/v0.1/hansard/entries/1147405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1147405,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147405/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kujiunga pamoja na wewe na Seneta wenzangu wahudumu wa maktaba kutoka kaunti zilizotajwa. Maktaba ni kiungo muhimu cha elimu na vile vile cha taasisi tofauti tofauti ili kuweza kujua tunatoka wapi na tunaenda wapi. Yale watakayo soma hapa itasaidia pakubwa kuweza kutengeneza maktaba na makavazi mazuri kwa vizazi vijavyo. Hapa Bungeni tuna utalaamu mwingi na vitabu na stakabadhi nyingi ambazo zitasaidia pakubwa kutuelimisha sisi kama Maseneta na watu wengine kuhusiana na taratibu za Bunge na mambo mengine kama hayo. Kwa hivyo, kusoma kwao na kuhudhuria kwao vikao hivi itasaidia pakubwa kuweza kujenga elimu na pia kueneza uhusiano mwema kati ya Bunge letu la Seneti na zile kaunti ambazo zimetutembelea. Karibuni na asante Bw. Spika wa Muda."
}