GET /api/v0.1/hansard/entries/1147411/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147411,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147411/?format=api",
"text_counter": 36,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Kitu cha kwanza, ninaungana na wewe kuwakaribisha maafisa wanaofanya kazi katika serikali za ugatuzi. Maafisa hao 31 wameingia katika Bunge la Seneti ili kujionea hali inavyoendelea. La muhimu ni kwamba hawa wafanyakazi katika maktaba wamekuja hapa kujionea na kupata faida ya kusoma na kujua jinsi ya kuendeleza maktaba huko wanakofanya kazi. Cha muhimu ni kuona watakaporudi wanakotoka, wataenda na elimu ambayo itawafaa katika kazi zao. Ninaona watu 31 lakini niko na imani pengine wale waliobaki, pia watapata nafasi ya kuja. Nimeangalia hii orodha nikaona wanatoka kaunti 31, lakini katika hii orodha, Kaunti ya Kilifi haipo. Niko na imani ya kwamba Kaunti ya Kilifi itakuwa katika raundi ingine itakayokuja. Jambo lingine la muhimu ni kuona ya kwamba serikali zote 47 za ugatuzi zimeamka. Kila kaunti inatakikana kuiga mfano huu na kuwa na maktaba yao ambayo itaweza kuwasaidia. Maktaba hizo pia zitasaidia waakilishi wa wadi mbalimbali kujinufaisha na elimu bora ambayo itawawezesha kusaidia serikali zao kuwa na nguvu zaidi. Wanapojisomesha na kujifahamisha kuhusu utendakazi wao, watakuwa bora zaidi kuliko vile walivyo sasa. Bw. Spika wa Muda, umefanya jambo jema kuwakaribisha hawa kuja kuona vile Seneti inafanya kazi na kuona vile Bunge linaendelea. Nina uhakika katika hizi siku tano ambazo watakuwa hapa, wakirudi nyumbani, wataweza kuona faida ya kuja hapa kujisomea mambo ya maktaba katika Bunge letu la Seneti."
}