GET /api/v0.1/hansard/entries/1147436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147436,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147436/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nataka kuongeza kidogo nikisema ya kwamba wale waliotengeza barabara walikuja hapa Kenya wakapata kwamba kuna barabara zake tayari. Walitoboa mashimo, na kutengeneza barabara yao nzuri sana. Mimi nishawahi kuipitia. Lakini sasa, waliharibu barabara ya chini. Kuna umuhimu ya kwamba anayeharibu ndiye anayetengeza. Ninaona kuna mushkil hapo ya watu fulani kutaka kuingia katika mambo ya ufisadi; Hizo Kshs9 billion ni pesa za Wakenya walalahoi ambao wanajaribu sana kuishi katika hii inchi ambayo imekuwa ghali kwa watu kuishi. Tunataka kujua ni kwa nini wanauliza swala la kuongezwa pesa za Kshs9 billion ili kutengeza sehemu ambayo iliharibiwa na wale waliopewa hiyo contract waitengeneze. Bw. Spika wa Muda, tumekuwa na ufisadi sana Kenya hususan Wizara ya Barabara. Kama mtu yeyote anataka kuwa tajiri, anaenda katika upande wa kutengeza barabara na tumeona hiyo ikitendeka. Watu wanaotengeneza barabara wamekuwa matajiri wa kupendukia, huku Mkenya wa kawaida akiendelea kukandamizwa na kuwa maskini hohehahe. Hivi sasa tuna barabara ya Nairobi Express Way ambayo tunalipa pesa nyingi kuitumia. Ukienda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), ukirudi, ukitoka na ukiingia ndani ukiwa unaenda sijui pande gani na gani, utatumia elfu kumi kwa siku mbili. Bei hii ni ghali muno. Bw. Spika wa muda, nakuambia wazi ya kwamba ufisadi wa namna hii, sisi kama Wakenya hatuwezi kuukubali. Lazima kuwe na sababu mwafaka ambazo zitaeleza vizuri ya kwamba hizi pesa wanazohitaji Wakenya kulipa ni za kazi gani. Nampa Sen. Cherargei heko kwa sababu ya kuangazia suala hili. Tuanataka kujua ni kwa sababu gani hii kampuni kama bado iko na sasa wananendelea kuwatoza Wakenya pesa. Je hizo pesa wanachukua kutoka kwa Wakenya watazitumia kutengeneza barabara ilioko chini ambayo wameharibu kabisa? Asante, Bw. Spika wa Muda."
}