GET /api/v0.1/hansard/entries/1147442/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147442,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147442/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii., Najiunga na Sen. Cherargei katika maombi yake ya taarifa kuhusiana na barabara ya Mombasa Road. Zabuni ya ile barabara ya moja kwa moja yaani Nairobi Express Way, ni tofauti na zabuni ya kurekebisha barabara ambayo ilikuwako hapo awali; Mombasa Road. Haiwezekani kwamba zabuni hiyo itolewe bila ya kufuata sheria. Sheria inasema kwamba zabuni zozote za barabara zinazohusu fedha nyingi ni lazima ziende kwa mipango yote ya zabuni. Kwa mfano, kutangazwa kwa kandarasi ili yeyote ambaye ana uwezo wa kufanya kazi ile aweze kupewa nafasi ya kuifanya. Bw. Spika wa Muda, hii barabara ya moja kwa moja imejengwa kwa mfumo wa jenga, endesha na baadaye itaachwa mikononi mwa Serikali. Kwa hivyo itakuwa ni makosa na ubadilifu wa fedha kuwacha zabuni kama hii kufanywa bila ya kufuata sheria. Hii taarifa ni muhimu sana. Ningeomba Kamati ya Barabara na Usafiri iangalie kwa makini na haraka kwa sababu muhula wa Bunge hili unaenda kuisha. Hii ndiyo fursa ambayo watu wanao fanya kazi katika Serikali kuweza kupata nafasi ya kupitisha zabuni ambazo hazina kichwa wala mguu ili kufanya ubadilifu wa pesa. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}