GET /api/v0.1/hansard/entries/1147481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1147481,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147481/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninasimama kwa hoja ya nidhamu. Ikiwa yule ambaye anazungumziwa hayuko ndani ya Bunge wala hajaitwa Bungeni na kuulizwa kisha akashindwa kujibu, mtu anaweza kusema alimwuliza na hakuweko? Je, ni haki? Waziri wa Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Vyama vya Ushirika, hayuko hapa. Katika mjadala unaoendelea hivi sasa, ndugu yangu anamtaja. Singependa kabisa kumuingilia kati rafiki yangu, mdogo wangu ambaye ninampenda sana na tunasikizana zaidi. Ni haki kuongea juu ya mtu ambaye hayuko ndani ya Bunge kwa njia ambayo haifai, ama kumwonyesha katika Taifa ya kwamba pengine si mtenda kazi maalum? Watu wengine kama sisi tunajua yeye ni mtendakazi. Je, ni sawa kuongea kama hayuko hapa ama si sawa?"
}