GET /api/v0.1/hansard/entries/1147653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1147653,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1147653/?format=api",
"text_counter": 278,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bwana Spika wa Muda, mwacha asili ni mtumwa. Sote kama Waafrika tukona asili zetu tofautitofauti. Ukiniambia niwache pombe ya mnazi itakuwa si sawa. Ijapokuwa mimi si Mmaasai lakini naishi naye kila siku nikiingia na nikitoka pia. Yeye ni ndungu yangu na rafiki yangu. Nimeenda ambapo amezaliwa, Kijiji kile na mahali familia yake yote ip, naijuwa. Katika miendendo na asili za wa-Maasai fimbo ni mmojawapo ya nguo ambazo wanazovaa. Huwezi kua Maasai na ukawa mikono yako ni mitupu kama hii yangu. Uamuzi uliotoa kwamba kinaweza kuwa kifaa hatari, si rahisi sana Wamaasai kuwa na hasira za kuanza vita. Labda awe amechokozwa ama amefanyiwa kitendo cha uhasama ili achukuwe hatua kama hiyo. Fimbo ni mojawapo wa nguzo za Kimaasai na ni sehemu ya mavazi. Tukisema hakiruhusiwi ndani ya hili Seneti nafikiria itakuwa ni makosa. Hapo awali, Spika mwenzako alitoa uamuzi huo na kusema kuwa moja katika nguo wanazovaa, taratibu na hisia zao, fimbo ya mkononi ni mojawapo wa mavazi ya Kimaasai. Asante."
}