GET /api/v0.1/hansard/entries/114769/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 114769,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/114769/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kubwa na hivi sasa, ni bahati kubwa kwa Bunge hili la Kumi kupata fursa na kuwapatia Wakenya kitu ambacho wametarajia kwa miaka 20 iliyopita. Katiba mpya ilitarajiwa miaka 20 iliyopita; Kenya nzima, pembe zote zilivyo, hakuna kitu muhimu leo kushinda kuwapatia Wakenya Katiba mpya. Kwa hivyo, Bunge hili, kupitia kwa Kamati hii ya Abdulkadir, ambayo imefanya kazi nzuri; ni Kamati ya Bunge hili; inayofaa watu waipongeze sana. Pia, inafaa watu walipongeze Bunge hili likiongozwa na Spika, Bw. Marende, na jambo hilo litaingia katika historia ya taifa hili la Kenya kwa sababu itakuwa ni mara ya pili kwa Wakenya kupata Katiba ambayo wanahitaji. Kitu cha pili ambacho nataka niseme hapa, Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kutambua juhudi ya Serikali ambayo iliyofanya katika mkasa wetu wa moto uliotokea katika kijiji changu cha Faza. Nataka kumpongeza Rais, Mhe Mwai Kibaki; nataka kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe Raila Odinga, kwa ule umuhimu walioichukulia kazi hiyo ili kuweza kuwanusuru wale waliopatikana na mkasa huo; walikuja haraka iwezekanavyo, chini ya wiki moja, na kuweza kuchangisha pesa zisizokuwa chini ya Ksh60 milioni. Hilo ni jambo ambalo limewatia moyo watu wangu wa Faza Rasini. Mimi mwenyewe ndio nilisimamia jambo hilo; nilizungumza na hawa viongozi wetu wa kitaifa wote wawili na wakanikubalia. Hivi sasa, ni wajibu wangu kutambua juhudi hiyo iliyofanyika. Ijapokuwa pesa zilizopatikana hazikutosha kwa sababu mkasa ulikuwa mkubwa-nyumba zilizochomeka zilikwa zaidi ya 400, tunashukuru hivi sasa, tunaipongeza pia ile Kamati iliyochaguliwa, kwa sababu karibu nyumba 60 au 70 tayari zimejengwa. Nataka kuchukua nafasi hii kumuomba Waziri wetu wa Fedha, Mhe Uhuru Kenyatta, atuchangie pesa za kutosha kupitia kwa Wizara yake ili tuweze kumaliza kazi hiyo iliyoko mbele yetu. Sisi tunahitaji kupata zaidi ya Kshs200 milioni. Kulingana na kazi ambayo iko mbele yetu, hiyo ni pesa kidogo. Tunafahamu kwamba Serikali yetu inatumia mabilioni ya pesa kuwasaidia Internally DisplacedPersons (IDPs). Hizo ni pesa nyingi sana. Ni haki kuwasaidia wale ambao hawako katika makao yao kwa kutumia mabilioni ya pesa. Lakini itakuwa muhimu pia ikiwa Serikali itatupatia pesa kupitia makadirio ambayo Waziri ataleta hivi punde. Mimi nimemwomba na kumwonyesha umuhimu wa kumaliza kujenga nyumba zilizoharibiwa na moto kule Faza. Pili, ningependa kuipongeza Serikali kwa juhudi zake za kutaka kujenga mradi mkubwa katika eneo hili la Afrika ya Mashariki na Kati. Mradi huo si mwingine bali ni"
}