GET /api/v0.1/hansard/entries/114770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 114770,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/114770/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ujenzi wa bandari ya pili katika taifa hili kule Lamu. Mradi huo utawaletea watu wa Lamu mafanikio makubwa. Ni matarajio yetu kwamba mradi huu ukitekelezwa basi barabara ya kutoka Mokowe hadi Kiunga itarekebishwa na kutiwa lami. Hili ni jambo ambalo tumelisisitiza siku nyingi sana. Ni nia yetu kwamba japo haya yote yako katika mipango ya Serikali, tungependa ianze kazi hiyo mwaka huu wala si mwaka ujao. Ningependa kumpongeza Waziri wa Kawi kwa sababu nilimwomba atufikishie umeme Kiunga kupitia mpango wa Rural Electrification, akatuahidi na labda kazi ya kusambaza umeme tayari imeanza kule. Mambo yanayohitajika kufanywa ni mengi lakini ikiwa binadamu atayapata hata machache, basi anapaswa kuyatambua na kutoa shukurani. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuchukua fursa hii kuongea machache kuhusu mipangilio ya fedha za CDF. Pesa za CDF zinafanya kazi nzuri kwetu. Kwa mfano, zimetumiwa kujenga shule za kutosha. Wakilisho langu la ubunge lilikuwa na shule ya upili moja lakini sasa tumejenga shule ya upili katika tarafa ya Kizingitini na watoto wanaendelea kusoma. Pia, tumejenga shule nyingine katika Tarafa ya Kiunga. Kazi hii yote inayofanywa kwa kutumia pesa za CDF. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hotuba ya Rais. Tuendelee kuwa na umoja. Vile vile, inafaa tuwahimize viongozi wetu wawili washauriane kwa mambo yote ili taifa hili lipate maendeleo ya kutosha."
}