GET /api/v0.1/hansard/entries/114790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 114790,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/114790/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hotuba ya Rais, ambayo naiunga mkono rasmi, na hususan maneno yenye uzito aliyoeleza na kutaka kushughulikiwa kwa dhati na sisi Wabunge wa Bunge la Kumi. Ningependa kuyanukuu maneno mazito aliyoyataja kwenye Hotuba yake. Changamoto zilizojiri katika siku hizi za majuzi, twataka ziangaliwe kwa makini sana."
}