GET /api/v0.1/hansard/entries/114792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 114792,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/114792/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "Jambo ambalo wananchi wanaliona lina uzito sana kwetu sisi Wabunge na Serikali kwa jumla ni ufisadi. Ingawa kwenye Hotuba yake Rais alitaja maneno ya kuwatia moyo wananchi, mara nyingi inaonekana kwamba kunapotokea visa vya ufisadi Serikali husahau kutekeleza majukumu yake ya kuwashtaki wale wanaofanya ufisadi. Bw. Naibu Spika wa Muda, mara kwa mara, tunakumbushwa ufisadi uliotokea wakati wa Goldenberg, Anglo Leasing, ufisadi wa mahindi, mafuta na, hata hivi majuzi, ufisadi wa fedha za elimu ya bure kwa shule za umma. Hayo ni mambo ambayo yameregeza nyuma imani ya wananchi wetu kwa Serikali yetu kwa hivi sasa. Jambo la kufurahisha ni kwamba kuna hatua ndogo iliyochukuliwa dhidi ya watuhumiwa fulani. Waliambiwa wakae kando kwa miezi mitatu ili wachunguzwe kulingana na ufisadi huo."
}