GET /api/v0.1/hansard/entries/114794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 114794,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/114794/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "vya watu binafsi, halafu viwanda hivyo viyachukue maziwa yale na kuwapelekea wanafunzi shuleni na maeneo ambayo yanahitaji maziwa wakati huu. Hilo ni jambo ambalo limewafanya wananchi kuwa na masikitiko makubwa. Kuna wale wenzetu wanaoitwa Internally Displaced Persons (IDPs). Wangepelekewa maziwa yale kwa gharama ya Serikali. Bw. Naibu Spika wa Muda, Rais pia alieleza kwenye Hotuba yake kwamba kila Mkenya aheshimiwe. Hili ni jambo la msingi wa Katiba yetu. Lakini ukija kwenye maswala ya kutolewa kwa vitambulisho, mara nyingi sisi watu wa Pwani hulalamika. Tunaona kwamba katika maeneo mengine ya Kenya, kuna sera tofauti za kutolewa kwa vitambulisho. Kwetu Pwani, sera inayotumika ni nyingine. Kijana akiwasilisha ombi la kusajiliwa, huulizwa amesoma wapi, anatakiwa aonyeshe kadi ya chanjo inayoonyesha hospitali aliyozaliwa. Pia anatakiwa aonyeshe birth certificate na kitambulisho cha babake, pamoja na vitambulisho vya babu yake, mamake na babake mamake. Katika maeneo mengine, mtu akifikisha umri wa miaka 18, haulizwi maswali kama hayo. Hili ni jambo ambalo tungependa Wizara inayoshughulika na maswala ya vitambulisho itueleze wazi mrengo na mfumo wa Kenya nzima, isiwe katika maeneo fulani, kuna mrengo mwingine na katika maeneo fulani kuna mrengo mwingine. Lakini tunaunga mkono wageni wasiweze kupata vitambulisho, pasipoti na vyeti vya kuzaliwa. Wale ambao tuna hakika ni Wakenya, kwa sababu tumezaliwa na tunaishi nao, wasisumbuliwe. Hivi sasa, ofisini kwetu, tuna watu zaidi ya 20 waliosubiri kwa zaidi ya miaka miwili bila kupata vitambulisho vyao. Tunataka Idara ya Mahakama ifanyiwe marekebisho. Zile kesi zinazopelekwa kwa Idara ya Mahakama zinachukua muda mrefu sana. Watu hawawezi kupata haki zao ikiwa muda wa kungoja haki itendeke utakuwa mrefu mno. Kuanzishwa kwa elimu ya bure katika shule za umma ni fikira nzuri sana kutoka kwa Serikali iliyopita. Mpango huo umewasaidia wananchi wengi sana, hasa wale wanaotoka kwenye maeneo yaliyoathiriwa na umaskini. Lakini masikitiko ni kwamba idadi ya walimu ni ndogo sana. Pia, madarasa yamekuwa machache sana. Vile vile, idadi ya vitabu vya kusoma imepungua sana kwa sababu wanafunzi wamekuwa wengi. Darasa lililokuwa na wanafunzi 40, leo lina wanafunzi 75 au 80. Pia, idadi ya walimu na madarasa haijaongezwa. Pesa ya kununua vitabu vya kusoma imekuwa shida kupata. Katika maswala ya kiuchumi, hakika tunapata upinzani mkubwa sana kutoka kwa nchi zetu jirani. Jambo moja ambalo limechangia kwa upinzani huu ni gharama ya umeme. Gharama ya umeme inawafanya wafanyabiashara watorokee nchi jirani. Wengine wanahamia Misri kwa sababu ya gharama ya umeme na maji. Ingawa kwetu tunaishukuru Serikali kwa upande wa barabara, kuna kilomita 80 kutoka Malindi hadi Lamu inafaa irekebishwe ili biashara iimalike. Bw. Spika wa Muda, iwapo Serikali itakuja na mfumo mpya wa kuweza kupunguza gharama za umeme, ninafikiri watu watapendelea kuja kufanya kazi na biashara hapa nchini kwa sababu ya hali ya bandari tulionayo. Tuko na barabara na reli hadi Uganda lakini kuna haja kubwa kwa Serikali kupunguza gharama za umeme kwa haraka. Pia, inafaa maswala ya maji yaangaliwe. Kwetu Pwani, wenye hoteli wanafanya fujo sana kwa sababu ya shida za maji ambazo zaweza kufanya wageni wakimbie. Kwa hivyo, ni bora kuangalia maswala ya maji kule Pwani."
}