GET /api/v0.1/hansard/entries/1148764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1148764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1148764/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kwamboka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 9246,
"legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
"slug": "beatrice-kwamboka-makori"
},
"content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuchangia huu Mswada wa Sen. Khaniri. Huu Mswada ni kitu ya maana sana kwa sababu hili janga si la Kaunti la Vihiga pekee yake; hii ni janga ambayo inaegemea kaunti zote kwa sababu hii Misaada inatolewa lakini kazi huwa haifanyiki kwa njia nzuri. Ukiangalia hii kazi ya mataa kwenye mabarabara utapata hii mataa inawekwa kwa njia isiyofaa. Unapata mataa mengi yanazima. Mataa yakizima mambo ya usalama katika kaunti zetu inakuwa mbovu kwa sababu hapo ndipo tunawezapata hawa vijana wahalifu, wanakuja kuvamia watu na maboma."
}