GET /api/v0.1/hansard/entries/1148766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1148766,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1148766/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kwamboka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 9246,
"legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
"slug": "beatrice-kwamboka-makori"
},
"content": "ni mbaya na mara nyingi tunapata watoto wetu na akina mama wakikanyaga maji taka ambayo inatoka kwa hiyo drainage system. Hii ni hasara kwetu kwa sababu unahitaji pesa pia kwenda kugharamia katika mahospitali. Wakati huu swala ni: Gavana wa Kaunti ya Vihiga anafanya kazi gani kwa sababu wakati huu anafaa kuwa amemaliza kazi kwa sababu tunaelekea muhula mwingine na uchaguzi mwingine? Inafaa kila gavana anayechaguliwa katika kila kaunti ahakikishe ile pesa inatoka katika Serikali ya Kitaifa kuteremka huko kwenye kaunti inafanya kazi inavyopaswa kufanyika. Hii pesa sio ya magavana wala mawaziri, ni pesa yetu sisi Wakenya na kama inakuja kwenye kaunti wacha ifanye kazi ambayo inastahili kufanyika. Bi Spika wa Muda, ningeomba hii Statement ikienda kwenye kamati, waweze kuingalia vizuri na kama watapata muda waende kule wahakikishe kuangalia kama ilifanyika ama haikufanyika. Kama haikufanyika wachukue hatua inayotakikana ili iwe funzo kwa magavana wote wa kaunti, ili wafanyie Wakenya kazi kwa njia ipasavyo. Asante Bi Spika wa Muda."
}