GET /api/v0.1/hansard/entries/1151849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1151849,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1151849/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu wa kudhibiti uchafu katika maeneo yetu. Niruhusu nikupe kongole kwa kutuwezesha kuwa na Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili. Sikupata fursa ya kukupongeza kwa sababu nilikuwa safarini. Sasa kwa vile tuna Kanuni za Kudumu kwa lugha ya Kiswahili, tungependa pia Miswada, ripoti na Taarifa zichapishwe kwa lugha ya Kiswahili. Hii itasaidia watu wanaofuatilia mijadala katika Bunge kusoma ripoti zetu kwa njia ya urahisi. Pia, itasaidia pakubwa kukuza lugha ya Kiswahili. Tulipokuwa tunaanzisha hizi Kanuni, lugha ya Kiswahili ilikuwa imeratibiwa kwa lugha inayotumika pakubwa ulemwenguni. Swala hili tulilofanya wakati ule lilisaidia pakubwa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na kutumika ulemwenguni. Mswada huu wa usimamizi wa uchafu umekuja kwa wakati mwafaka. Tumeona kwamba kaunti zetu zinapata shida na lundo la takataka. Tumeona Kaunti ya Kisumu imeweza kudhibiti taka zao kwa njia ambayo inaleta usafi kwa mji wao. Vilevile, Kaunti ya Mombasa, tumefanya hivyo. Zamani, ulipopita Kibarani, lazima ungefunga mapua yako. Sasa ukipita kibarani ni kusafi, kumepandwa miti na kumewekwa vinyago vya wanyama ambapo Jumapili watu wanakwenda kujivinjari. Watu wengi wanazuru sehemu ile kuona yale mabadaliko makubwa ambayo yamefanyika. Ya kusikitisha ni kuwa jaa lingine la taka limepelekwa mtaa wa makaazi wa VoK, Nyali. Jaa hili limeweza kukua mpaka sasa limekuwa ni shida kulidhibiti. Ijapokuwa jaa kubwa la Mombasa liko sehemu ya Mwakirunge, lakini hili ambalo liko katika eneo la VoK limekuwa ni udhia kwa wakaazi wengi wa Nyali na sehemu hiyo. Naomba Serikali ya Kaunti ya Mombasa iweze kuhakikisha ya kwamba jaa lile limeondolewa pia. Hii ni kwa sababu hatuwezi kuwa na jaa katikati ya makaazi ya watu. Usafi ni ustaarabu. Naweza kuleta sheria kama hii, lakini ikiwa sisi wenyewe hatuna ustaarabu wa kuwa wasafi ama kuweza kudhibiti takataka zetu hata tuwe na sheria kama hii haitasaidia. kwa mfano, tumewaona watu wengine wanaendesha magari barabarani na wakikunywa maji, wanarusha chupa nje na kuanguka kwenye barabara. Kwa hivyo, hata ukamuekea sheria mtu kama huyo, itakuwa ni kama kupigia mbuzi"
}