GET /api/v0.1/hansard/entries/1151851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1151851,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1151851/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "guitar kwa sababu, hana tabia ya ustaarabu. Kwa hivyo, kama huna tabia ya ustaarabu, hata ukawekewa sharia, haitakuwa na faida yoyote. Sheria hii itasaidia pakubwa kudhibiti lundo la *takataka katika kaunti zetu. Sheria hii pia itadhibiti kuagizwa kutoka kwa nchi za nje takataka ama mabaki ya vitu vichafu kama vile vitu vya sumu. Tukikumbuka hapo awali eneo la Mikindani, Kijiji cha Owino Uhuru wakaazi walienda mahakamani kudai ridhaa kwa sababu walikuwa wameletewa mabaki ya madini ya lead ambayo yalikuwa na sumu na yakaathiri afya zao. Serikali ikaombwa ilipe Ksh3 bilioni mwaka uliopita. Lakini, mpaka sasa, pesa hizo hazijalipwa. Ijapokuwa athari zile zimepungua, watu wa Owino Uhuru Kaunti ya Mombasa wanazidi kupata shida kwa sababu zile pesa zingewasaidia kugharamia matibabu na mambo kama hayo. Jambo lingine limenifurahisha ni kuwa hii sheria ikipitishwa katika Bunge hili, serikali za kaunti zitalazimika kupitisha sheria hii ili kudhibiti takataka katika maeneo yao. Mara nyingi taka hizi zikibebwa, zinatupwa maeneo fulani ambayo inakuwa ni hasara. Watu wanaokota taka katikati ya mji na kutupa katika eneo fulani ambapo zinachomwa. Zikichomwa zinaharibu mazingira kwa sababu ule uchafu ukiingia hewani unaharibu ozone layer. Hii inasababisha kubadilika kwa hali ya anga. Hili imekuwa tatizo kubwa katika ulimwengu. Hii inasababishwa pia na maswala ya kuchoma taka ovyoovyo. Haya maswala ya kuchoma taka yanatakikana yasimamishwe ile tukae kwa mazingira safi. Matumizi ya takataka hizi uleta bidhaa tofauti. Kwa mfano, kuna nchi ambazo zinapata nguvu za umeme kutokana na takataka na vitu ambavyo vinatupwa. Tumeona kuna sehemu zingine taka inaundwa kuwa vitu tofauti kama makaa ya kupikia na matofali ya kujenga pia. Zote hizi zinafanyika iwapo kutakuwa na uwekezaji katika sekta hii ya taka. Wengi ambao wametumia takataka kwa njia nzuri, wamepata manufaa makubwa. Badala ya kuchukua taka na kuchoma, itakuwa ni bora kaunti zetu ziweze kulazimishwa kuhakikisha kwamba hizi takataka zinatumika kwa njia ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuleta mazingira safi katika maeneo husika. Bw. Spika, katika sheria hii, kuna nafasi ya kutatua mizozo kupitia kwa uwiano ama mazungumzo. Kiingereza wanasema dispute resolution section ambayo ni kifungu cha 32 ya sheria hii. Hiyo itasaidia pakubwa kupunguza mizozo baina ya kaunti. Kwa mfano, takataks za Nairobi zilikuwa zinatupwa Murang’a. Kwa hivyo, mizozo kama hiyo haitakuwepo iwapo sheria hii itatutumika. Sheria hii ni nzuri. Kaunti zetu nyingi zinatumia sheria za miaka kumi baada ya kuwa na serikali za ugatuzi. Kaunti nyingi zinatumia bylaws ama sheria ambazo zilikuwa zimepitishwa na county councils za zamani, kudhibiti mambo ya takataka kama ambayo yamezungumziwa na sheria hii."
}