GET /api/v0.1/hansard/entries/1152944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1152944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1152944/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili nitoe risala za rambirambi kutoka kwangu, jamii yangu, na Eneo Bunge la Taveta kwa ujumla. Rais wetu wa tatu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwai Kibaki, alikuwa si Rais tu, bali pia baba mpendwa wa watu, mpenda maskini na wa kuhakikisha kuwa maskini wameinuliwa juu. Nilipata fursa ya kufanya kazi naye kwa ukaribu. Hata nilipokuwa katika upinzani, kila mara alipenda kusikiza na kututatulia shida zetu za Taveta. Vilevile, niliporudi awamu ya pili, tulifanya kazi naye akiwa Rais wangu. Vilevile, alinipa nafasi ya kuwa katika Baraza lake la Mawaziri."
}