GET /api/v0.1/hansard/entries/1153263/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1153263,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1153263/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninaungana na wewe kutoa rambirambi. Ningependa pia kutoa rambirambi kwa niaba ya familia yangu na hususan watu wangu wa Kaunti ya Kilifi ambao walinipa nafasi hii kuwaakilisha katika Bunge la Seneti. Rambirambi ziwaendee watu wa Kaunti ya Nyeri, eneo Bunge la Othaya na familia ya mwendazake, marehemu Mwai Kibaki. Kitu cha maana cha kumkumbukia marehemu ni ushupavu wake katika mijadala Bungeni. Katika historia ya wanasiasa waliokuwa Bungeni, yeye alikuwa mmoja wao wa kipau mbele. Alikuwa Bungeni kwa zaidi ya miaka 50. Bi. Naibu Spika, wewe na mimi tunaelewa ya kwamba kuketi kwa hili Bunge kwa miaka 50 ni kwamba umechaguliwa mara 10 na wananchi. Ninampa kongole kwa mfano mzuri ambao ulimwezesha kuchaguliwa kwa mihula kumi. Ikiwa muhula mmoja ni miaka mitano, mihula 10 ni miaka 50. Ni jambo ambalo sisi wengine hatujui ikiwa tunaweza kufanya. Aliweza kufanyiwa hivyo kwa sababu ya ujasiri wake. Bi. Naibu Spika, cha kwanza, lazima tuangalie na kuzingatia huyu Rais Mwai Kibaki alikuwa mtu wa aina gani. Alisomea Shahada la Uchumi wakati ambapo watu wachache sana walikuwa na hii Shahada. Alikuwa mmoja wa waliotambuliwa ulimwenguni kwa taaluma ya Uchumi, ambayo ingemwezesha kuwa kiongozi na kusaidia nchi yake. Bi. Naibu Spika, tunakumbuka alipochukua hatamu za uongozi, benki zilifungua milango na watu kuitwa wachukue mikipo. Kabla ya yeye, kupata mkopo ilikuwa ni vigumu. Baada yake, tumerudi palepale ambapo ni ngumu kupata mkopo wa benki. Jambo la kushangaza ni kwamba wakati wa Rais Mwai Kibaki, magazeti yalikuwa yakichapisha kwamba aliye na haja na pesa aende achukue. Ninakumbuka wakati huo uchumi u likuwa mzuri kwa sababu watu walijinufaisha kwa mikopo. Hivyo basi, watu waliweza kuendelea kwa sababu uchumi ulikuwa bora. Mimi binafsi nilifanya kazi na Rais Mwai Kibaki kwa muda wa miaka mitatu. Tulifanya kazi kwa karibu sana. Ninasema hivyo kwa sababu, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}