GET /api/v0.1/hansard/entries/1153266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1153266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1153266/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "pamoja na yeye. Hilo ndilo gari ambalo tulikuwa tukitumia kuzunguka wakati wa kufungua maonyesho ya ukulima. Huo ndio wakati ambapo nilikuwa karibu naye na nikajua alikuwa mtu wa aina gani. Alipenda nchi yake na alihisi kwamba lazima wakulima wasaidiwe. Ninakumbuka ni wakati wake ambapo bei ya mbolea ilishuka chini. Wakulima waliweza kumudu bei ya mbolea; walilima na nchi ikawa na mazao tele. Wakati wa Rais Kibaki, hapakuwa na baa la njaa jinsi ambavyo watu wanaaga kwa njaa siku hizi. Rais Kibaki alifungua uchumi na kuwapa wakulima mbolea kwa bei nafuu ili wakuze chakula cha kutosha nchi nzima. Bi. Naibu Spika, nikimalizia, ningependa kusema kwamba wakati wowote Serikali ilipofikiria kutengeneza barabara za Pwani, ilikuwa inafikiria watalii wala sio watu wa Pwani. Wakati alipochukua hatamu za uongozi, aliamua watu wa Pwani wanahitaji barabara. Alitambua kuwa barabara nzuri ingewezesha wakulima kufikisha mazao yao katika soko la Marikiti na masoko mengine, kabla ya kuharibika. Barabara moja ambayo tutamkumbukia ni ile ya kutoka Malindi hadi Mombasa. Barabara hiyo ilipanuliwa na ikasaidia watu wengi sana. Tukiangalia upande wa elimu, tulikuwa tunafikiria haiwezekani watoto kusoma bila kulipa karo. Hata hivyo, ilikuja ikatokea. Maajabu ni kwamba uchumi ukiwa bora, mambo mengi yanatengenezeka. Rais Kibaki alionyesha mfano bora wa uongozi na mambo ambayo unaweza kufanya ukiwa kiongozi wa Taifa. Ndio sababu watoto waliweza kusoma pasipo kulipa karo, na tunamshukuru kwa hilo. Bi. Naibu Spika, ninataka kuwachia hapo. Kuna mengi ya kusema na watu watamkumbuka mwendazake. Sisi kama viongozi katika hii inchi, tuige mfano wa marehemu Emilio Mwai Kibaki. Nawaambia wale watoto wake waliobaki ya kwamba waweze kushikilia familia. Letu litakuwa ni kuomba Mungu awajaze na imani wakati huu. Sisi tutazidi kuwaombea Mungu awape mwelekeo na waweze kuepukana na mtihani kama huu ili wapate nguvu; wao na wajukuu waweze kuwa na maisha bora mbeleni. Bi. Naibu Spika, la mwisho ni kwamba, ufisadi ulikuwa haupo katika orodha yake. Alipokuwa uongozini ufisadi ulikuwa umerudi chini sana. Hivi sasa tunaona ufisadi umechipuka zaidi. Tunaomba ya kwamba ikiwa kuna kitu chochote tunaweza kuiga, tuige mwenendo wa mwenda zake Rais Emilio Mwai Kibaki. Ikiwa yeye alikuwa hataki ufisadi, basi hivi sasa tunapoelekea kufanya uchaguzi wa Rais, tunamjua atakaye kuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}