GET /api/v0.1/hansard/entries/1154039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1154039,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1154039/?format=api",
"text_counter": 256,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu wa kuwa na Huduma Namba. Namshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa katika Bunge hili. Ni kweli vile wenzangu wamechangia, imekuwa vigumu sana. Hata leo asubuhi nimepigiwa simu na mtoto wangu kutoka Australia kwamba anataka cheti cha kuzaliwa. Tungelikuwa na kadi kama hii, mtoto hangepiga simu na kusema anataka kadi ya kuzaliwa. Tukiwa na kadi hii, itakuwa inabeba kila kitu. Naona mwishowe hii kadi itakuwa inabeba kila kitu. Naona hiyo kadi itakuja kusaidia watoto wetu iwapo wamefika kidato fulani. Mtu atajua huyo mtoto amesoma kutoka kidato fulani na akafika mahali fulani, ameenda kutoka shule ya msingi hadi shule ya upili, na hata chuo kikuu. Hili ni jambo la maana sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}