GET /api/v0.1/hansard/entries/1154040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1154040,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1154040/?format=api",
    "text_counter": 257,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Hapo awali, tukiwa wafanyakazi katika idara wakati tulitaka kulipwa mshahara, walikuwa wanaleta payroll wakitumia kalamu kuangalia jina lako. Unaona mahali tumefika. Benki zetu zinaweza kutuwekea hizo pesa. Iwapo tutakuwa na hiyo Huduma Namba, itarahisisha kila kitu na hivyo tutakuwa kama nchi nyingine. Mhe. Waluke amesema wale tuko kwa mipaka yetu tutafaidika. Ni kweli, hata ukija mahali panaitwa Suam kule Trans Nzoia, tuna ndugu zetu wanaotoka Uganda. Hata wakati huu tunapopiga kura, wenzetu wanaenda mpaka nchi za ng’ambo kuangalia wapigaji kura waje katika nchi yetu ya Kenya. Tukiwa na hiyo Huduma Namba ya kusema huyu au yule ni ndugu au jirani yetu na anakaa upande huu, itatuwezesha kupata viongozi sahihi wanaoweza kusaidia nchi hii na wale wanaweza kusaidia watu wetu walio mpakani. Itakuwa ni rahisi mno. Hata wakisema huko Mhe. Sankok anatoka, hao ni watu waliokuwa na utamaduni wao wa kuuza bidhaa zao. Wao ni wanabiashara. Mimi huona watu kutoka nchi za ng’ambo wakija mpaka huko Maasaini kufanya biashara na wao. Iwapo mtu ana hiyo kadi yake, inakuwa rahisi kujua anatoka wapi na anafanya nini. Namshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Usalama wa Taifa katika Bunge hili na nikushukuru wewe. Nakutakia heri na fanaka hata wakati tunapotafuta kura. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}