GET /api/v0.1/hansard/entries/1157333/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1157333,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1157333/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ni lazima Serikali ijifunge kibwebwe. Wananchi wanaofanya juhudi kuendeleza utalii wanafaa kutiwa moyo ili watie bidii zaidi ili kuzuia matukio ambayo yanaweza kuzuia maendeleo ya wananchi kwa sababu ya mkinzano kati ya wanyamapori na wananchi. Nasema hivyo kwa sababu pesa inayotokana na Mto Mara ni nyingi mno, hasa kwa Kaunti ya Narok. Kaunti zingine pia zinafaa kusaidiwa ili mbuga za wanyama zithibitiwe na wanyamapori wasiingie maeneo ya wananchi, kwa sababu kuna wananchi wanaojua umuhimu wa vivutio vya utalii kutokana na wanyamapori. Kwa hivyo, Serikali inafaa kujizatiti ili kupunguza kile tunachoita human-wildlife conflict. Bw. Spika wa Muda, tulikuwa jijini Geneva kwa Conference of the Parties (COP). Katika huo mkutano, ulimwengu wote uliamua kupunguza human-wildlifeconflict kunahitaji mambo mawili. La kwanza ni kujenga nyaya za stima ili kuweka kizingiti kati ya wananchi na wanyama pori. La pili lilikuwa kulipa fidia kwa wakati unofaa. Katika Bunge hili la Seneti, tulipitisha Wildlife Management Amendment Bill . Kitu cha kwanza ambacho tuiangazia kilikuwa kulipa fidia kwa wakati unao faa. Bw. Spika wa Muda, ninapoongea sasa hivi, kuna watu ambao kwa miaka mingi, ng’ombe na vyakula vyao vimeliwa na wanyama pori. Kuanzia mwaka wa 2013/2014 hadi sasa, hawajalipwa fidia. Langu ni kuambia Serikali ya kwamba tunafurahia ule ushuru tunaopata kutokana na utalii unaoletwa na wanyama pori. Hata hivyo, na wao pia wajizatiti kuweka nyaya za stima. Hii itasaidia watu wetu kwa kuzuia maangamizi yanayotokana na wanyama. Serikali pia ilipe fidia kwa wakati unaofaa. Katika ule mkutano uliokuwa jijini Geneva, watu kutoka nchi za Southern African Development Community (SADC), ambazo ni South Africa, Botswana, na Mozambique, waliuliza wakubaliwe kuuza pembe za ndovu ili walipe watu wao fidia kwa wakati unaofaa. Ule mkutano ulikataa kwa sababu ingepelekea kuuawa kwa ndovu zaidi. Sababu ni kwamba ni vigumu kutambua kama hizi pembe za ndovu zinatokana na wanyama waliokufa wenyewe ama kama wameuwawa."
}