GET /api/v0.1/hansard/entries/1157335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1157335,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1157335/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Katika huo mkutano pia, Japan iliuliza ikubaliwe kununua pembe za ndovu ambao wamekufa wenyewe. Ulimwengu pia ulikataa kuwapa ruhusa kwa sababu ingekua kama incentive ya kuwaua ndovu zaidi. Nashukuru kwa hii Statement na ningechangia ya kwamba tuendelee kulinda wanyama wetu kwa sababu ni kivutio kizuri cha ushuru unaotokana na utalii. Serikali pia ijizatiti ifunge buti ili kuzuia hiyo hasara inayoletwa na wanyama pori. Kule kwetu Kaunti ya Taita Taveta, wanaichi wa huko ni watu wenye bidii. Wanalima, wanafuga ng’ombe na tuko na range land zaidi ya ekari million 1.4 . Licha yahayo, hatupati faida yeyote kwa sababu wanyama pori wanakula ng’ombe, mbuzi na chakula cha wananchi. Mwaka uliopita tulisikuma kidogo tukapata fidia ya Kshs20 millioni. Lakini tunadai zaidi ya Kshs200 millioni kutoka kwa Serikali ya Kenya, ambayo hawataki kulipa wananchi wetu. Kuna muwaniaji mmoja wa kiti cha Useneta ambaye mojawapo ya sera zake ni kwamba akipigiwakura, atakuwa anaua ndovu. Anafikiria kwamba tukiua ndovu ndio tutapata manufaa. Ukweli ni kwamba, ndovu ni utamadanu wetu. It is part of ournational heritage. Kwa hivyo, Serikali lazima ifunge buti ili kutusaidia kwa hii Human-Wildlife conflict."
}